February 13, 2016



Mganda Hamisi Kiiza ameonyesha kweli amepania kufanya vema zaidi na kupachika mabao kila inapowezekana kuisaidia Simba.

Kiiza amefunga mabao mawili leo na kuisaidia Simba kushinda kwa 2-1 dhidi ya Stand United, sasa ndiyo vinara wa Ligi kuu Tanzania Bara baada ya kufikisha pointi 44.

Mabao hayo mawili, yamekuwa msaada kwa Simba lakini msaada kwa Kiiza ambaye amefikisha mabao 16 na kumpita mshindani wake mkuu katika upachikaji mabao, Amissi Kiiza wa Yanga mwenye 14.

Kiiza alikuwa akiitumikia Yanga nchini Mauritius katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Kuna nafasi ya kufunga katika mechi ijayo lakini tayari Kiiza aliyekuwa nyuma yake kwa mabao manne, sasa amempita.

Donald Ngoma ana mabao 10 sawa na Jeremiah wa Prisons na Elius Maguri wa Stand United ana 9 akiwa amekwama hapo muda mrefu sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic