October 19, 2017



Kikubwa anachokitaka Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioba ni kuhakikisha anazipiku Simba na Yanga.

Kiu ya Cioba raia wa Romania ni kukaa kileleni mwa Ligi Kuu Bara, nafasi ambayo anaamini inawezekana.

Ili kutimiza malengo yake, Cioba anataka kuanza na pointi tatu za Mbao FC.

Azam inayoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara wikiendi hii itakuwa na kibarua kigumu cha kucheza na Mbao kwenye mchezo wa ligi hiyo utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Azam imezidiwa na Simba na Yanga kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa ingawa wote wanalingana wakiwa na pointi 12.

Meneja wa Azam, Philipo Alando amesema kocha wao anataka kushinda mchezo huo kwa ajili ya kujitengenezea mazingira ya kukaa kileleni kabla wapinzani wao, Simba na Yanga hawajavaana Oktoba 28.

"Kocha amepanga tushinde mchezo huu na Mbao kwa ajili ya kujiwekea mazingira ya kukaa kileleni pale tutakaporudi kwenye uwanja wetu wa nyumbani," alisema Alando.

Hivi karibuni, Cioba alilalamika kuhusiana na viwanja vibovu vya mikoani baada ya Azam FC kwenda na mwendo wa sare ikiwemo ile dhidi ya Singida United mjini Dodoma, wao wakilazimika "kuchomoa".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic