December 14, 2017



Na Mwandishi Wetu
KOCHA Mkuu wa Yanga Mzambia, George Lwandamina, kesho alfajiri anatarajiwa kukwea pia kurudi kwao kwa ajili ya kusherekea mahafali ya mwanaye ambayo ni siku muhimu kwake kama mzazi.

Mzambia huyo, anaondoka huku akiacha timu yake ikiwa inajiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa keshokutwa Jumamosi saa kumi jioni.

Akizungumza na Salehejembe, Katibu Mkuu wa timu hiyo, Boniface Mkwasa alisema kuwa kocha huyo huyo aliomba ruhusa hiyo kwa viongozi leo asubuhi wakati timu hiyo ikiwa kwenye mapumziko ya mazoezi ya siku moja.

“Kocha wetu Lwandamina leo ameomba ruhusa ya kwenda mara moja kwa ajili ya kuhudhuria mahafali ya mwanaye yatakayofanyika wikiendi hii.


“Hivyo, ataukosa mchezo wa kirafiki tutakaoucheza keshokutwa Jumamosi na badala yake atakuwepo benchi msaidizi wake Nsajigwa (Shardack) na atarejea nchini Jumatatu ijayo asubuhi,” alisema Mkwasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic