May 23, 2013





Yanga imeanza harakati za kumuongeza kipa mpya ambaye atashirikiana na Ally Mustapha ‘Barthez’.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Yanga, zimeeleza Kocha Mkuu, Ernie Brandts ametaka kipa mwingine mzoefu ikiwezekana kutoka nje ya nchi aongezwe.

“Kocha anamkubali sana Barthez na kwa msimu mzima amefanya kazi nzuri sana, lakini ametaka aongezewe nguvu na amesisitiza apatikane kipa mzoefu.

“Brandts amesisitiza hata kama kipa atakuwa anatokea nje basi atafutwe na kujiunga na timu hasa kwa kuwa tunashiriki michuano ya kimataifa.


“Hivyo suala hilo tumeanza kulifanyia mikakati, ninaamini baada ya muda mambo yatakuwa mazuri kabisa,” kilieleza chanzo cha uhakika.

Kipa namba mbili Said Mohammed, amekuwa akionekana kutokuwa na nafasi zaidi, hali ambayo inaonyesha imemlazimu Brandts ambaye sasa yuko kwao Uholanzi kusisitiza aongezwe kipa mwingine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic