May 23, 2013




Kocha wa Simba, Patrick amerejea kwao nchini Ufaransa na kuna kila dalili ikawa ndiyo ‘safari’.

Kumekuwa na mjadala mkubwa ndani ya Simba kuhusu waendelee na Liewig au la.

Lakini mwenyewe ameliambia Salehjembe kwamba, bado anajiuliza kama ataendelea kazi na Simba au la.

“Ila ninawaachia wao, mimi niko tayari kuendelea, lakini wao ndiyo watamaliza kama ni mtihani maana wana majibu” alisema.


Kwa ufundishaji ameonyesha ni kocha mzuri lakini Liewig amekuwa mkali kupindukia.
Kingine ambacho amekuwa akilaumiwa ni kushindwa kufanya kazi kwa ufasaha katika suala la kuunganisha timu.

Hata hivyo, Simba wamekuwa wakiitumia ripoti yake kwa ajili ya kufanya usajili mpya.

Kocha huyo alichukua nafasi ya Mserbia, Milovan Cirkovic ambaye alikuwa kipenzi cha Wanasimba na inaonekana Liewig ameshindwa kuwa na ushawishi katika hilo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic