May 23, 2013


Muda baada ya kutua Dar kutoka Ujerumani..

 
Kinda wa Azam FC, Mudathir Yahya ameamua kusitisha mafunzo ya soka nchini Ujerumani na kujiunga na timu ya taifa, Taifa Stars.

Mudathiri amerejea nchini juzi na kujiunga na kambi ya Taifa Stars inayojiandaa na mechi dhidi ya Morocco kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

“Nimerudi kutoka Ujerumani, nimewaacha wenzangu wakiendelea lakini nimeona ni bora kurudi kwa ajili ya timu ya taifa,” alisema.


Mudathiri ameitwa katika kikosi hicho kwa mara ya kwanza lakini kabla ya hapo, Kim Poulsen alimuita katika Young Taifa Stars.

Kiungo huyo ni kati ya chipukizi wanaochipukia kwa kasi na kama ataendelea vizuri huenda akafika mbali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic