Straika Wayne Rooney ameendelea kubaki kwenye mipango ya Klabu ya Arsenal ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa klabu huyo, Ivan Gazidis amethibitisha juu ya taarifa hizo.
Arsenal ina imani kuwa ikitoa dau zuri la usajili na kumpa mchezaji huyo kiasi fulani cha fedha anaweza kuwa tayari kupokea mshahara wa pauni 170,000 kwa wiki kutoka ule wa pauni 250,000 anaolipwa Man United.
Wachezaji wengine ambao pia wanawaniwa na Arsenal ni pamoja na kiungo wa Everton, Marouane Fellaini.
Arsenal pia inawawania straika wa Fiorentina, Stevan Jovetic na Gonzalo Higuain wa Real Madrid lakini inaaminika kuwa kama ikikosa wote hao inaweza kumfikiria mshambuliaji wa Swansea, Michu.
Gazidis alithibitisha kuwa klabu yao imetenge kiasi cha pauni milioni 70 kwa ajili ya usajili. Timu hiyo haijatwaa ubingwa wowote mkubwa kwa miaka nane sasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment