Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amempa
onyo nahodha wa timu hiyo, John Terry kuwa anaweza kumuweka benchi kama ambavyo
alivyofanya kocha wa muda aliyepita klabuni hapo, Rafa Benitez kama hata
onyesha uwezo mzuri.
Mourinho ambaye ametua Chelsea hivi
katibuni akitokea Real Madrid, amesema kuwa atapanga wachezaji kwa kufuata
faida yao kikosini na siyo kuangalia jina la mtu.
Akiwa Real Madrid, kocha huyo
alimweka benchi bila huruma nahodha wa timu hiyo, Iker Casillas licha ya kuwa
alikuwa kwenye kiwango kizuri.
“Mimi ndiyo kocha, nitampanga
mchezaji kutokana na kiwango chake, mchezaji anapata nafasi anapoonyesha uwezo
mazoezini.
“Ilikuwa kawaida kwangu kumuacha (Marco)
Materazzi, ndivyo ninavyoweza kufanya kama alivyofanya Benitez mwaka huu kwa
Terry,” alisema Mourinho.
0 COMMENTS:
Post a Comment