Klabu ya Reading imefanikiwa kuwazidi
QPR kwa kufanikiwa kumsajili beki wa kushoto wa Manchester City, Wayne Bridge.
Bridge mwenye umri wa miaka 32 ambaye
aliwahi kukwakuruzana na John Terry wa Chelsea kutokana na Terry kufanya ngono
na aliyekuwa mpenzi wa mchezaji huyo, amekuwa huru baada ya mkataba wake na Man
City uliomwezesha kuvuna pauni 90,000 kila wiki kumalizika.
Bridge amekuwa akitumia muda mwingi
akiwa nje ya Man City lakini aligoma kuvunja mkataba wake, hivyo licha ya
kupelekwa timu nyingine kwa mkopo au kuwepo klabuni hapo huku akiwa hachezi,
bado aliendelea kupata mshahara wake kama kawaida.
Nina furaha kujiunga Reading naimani
nimefanya chaguo sahihi,” alisema Bridge na kuongeza:
“Nimezungumza na kocha na
amenielekeza nia yake ya kule timu anapotaka timu ielekee, amefurahishwa sana
na usajili wangu hapo.”
Kutokana na mvutano huo, Bridge
aligoma kumsalimia Terry kwa kutompa mkono wakati Man City na Chelsea
zilipokutana.
0 COMMENTS:
Post a Comment