September 4, 2013





Klabu ya Simba imepanga kutumia fedha zote za mapato katika mechi yao ya kirafiki ya juzi dhidi ya Mafunzo kwa ajili ya kumpeleka kiungo wao, Kiggi Makasi nchini India katika matibabu.

Timu hiyo ilivaana na Mafunzo juzi Jumatatu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam  na mchezo huo ulimalizika kwa Simba kushinda mabao 4-3.


Akizungumza na Championi Jumatano, Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi’, alisema kuwa fedha hizo za mechi zitatumika kwa ajili ya matibabu ya mchezaji huyo nchini India.

Mzee Kinesi alisema fedha hizo zote atapewa kiungo huyo.

“Maandalizi ya safari ya Kiggi kwenda nchini India tayari yamekamilika kutokana na kupatikana fedha za kumpeleka huko.

“Fedha hizo zimepatikana katika mapato ya mechi dhidi ya Mafunzo iliyochezwa hivi karibuni, hivyo mapato yote atapatiwa yeye na tunaamini yatasaidia katika matibabu yake,” alisema Mzee Kinesi.

Kiggi amekuwa akisumbuliwa na goti na timu hiyo ya Msimbazi ilimtoa kwenye usajili wake wa mwaka huu mpaka atakapopona.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic