Beki mpya wa Simba, Kaze Gilbert, ameumizwa na kitendo cha kuruhusu
mabao matatu katika mechi ya kirafiki waliyocheza juzi Jumanne dhidi ya Mafunzo
ya Zanzibar.
Huo ulikuwa mchezo wa kwanza wa Kaze kwa mashabiki wa Dar es Salaam kuichezea
Simba na vijana hao wa Msimbazi kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-3.
Kaze amesema kuwa idadi hiyo ya mabao ni kubwa kwake kutokana na uwezo
wake ndani ya uwanja.
Alisema amepanga kulidhibiti hilo ili katika mechi zijazo za Ligi Kuu
Tanzania Bara na mashindano lisijitokeze tena na anataka kuhakikisha kuwa timu
hiyo hairuhusu mabao mengi kiasi hicho kwenye mechi.
“Kama beki nimeumia sana kitendo cha kuruhusu mabao matatu katika
mechi ya leo (juzi) dhidi ya Mafunzo, hii ni idadi kubwa ya mabao kwangu.
“Mimi na mabeki wenzangu kiukweli tunahitaji kubadilika kwa kucheza
kwa pamoja ili kuhakikisha haturuhusu tena idadi kubwa ya mabao kama hiyo,”
alisema Kaze, raia wa Burundi, aliyesajiliwa na Simba msimu huu akitokea
Vital’O.
0 COMMENTS:
Post a Comment