Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts,
amekifanyia kazi kikosi chake wakati kikifanya mazoezi na akataja kile
anachopunguza kiungo wake Mrisho Ngassa katika timu hiyo.
Kauli hiyo ya Brandts inakuja kufuatia
Ngassa kufungiwa kuichezea Yanga mechi sita, baada ya kubainika kuwa na kasoro
katika mchakato wa usajili, ambapo mpaka sasa winga huyo mwenye kasi
ameshaikosa michezo mitatu ya klabu hiyo.
Akizungumza na Championi Jumatano mara
baada ya kumalizika kwa mazoezi ya jana asubuhi ya kikosi hicho yaliyofanyika
katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola jijini Dar es Salaam, Brandts
amesema hana wasiwasi katika ubora wa kikosi chake hicho lakini wanakosa mambo
mengi ikiwemo kasi na mbinu nyingi alizonazo Ngassa katika kuiongezea nguvu
timu yake.
Brandts amesema uwepo wa Ngassa katika
timu hiyo ni tishio kubwa kwa mabeki wa timu pinzani ambao wengi hushindwa
kujipanga vizuri kutokana na kasi ya nyota huyo. Katika hilo alimaanisha kwamba
kama angekuwepo katika kikosi hicho, washambuliaji wake wangeweza kufunga mabao
mengi katika kila mchezo.
“Nakosa vitu vingi kutoka kwa Ngassa,
mbio zake na mbinu nyingi ni kati ya vitu tunavyovikosa sasa kutokana na hii
adhabu yake, angalia nina timu bora lakini alikuwepo katika mipango yangu.
Kukosekana kwake sasa ni kitu
kinachoniumiza kichwa,” alisema Brandts huku akiongeza kwa kusema:
“Sina maana kama wachezaji wengine si
muhimu, hapana, ila kuna kila kitu kutoka kwa kila mchezaji, akiwa uwanjani
(Ngassa) hakuna beki anayeweza kuwa sawa kiakili kutokana na kasi na mbinu
alizonazo. Tunakosa mabao mengi ambayo angeweza kuwatengenezea wenzake
kulingana na uwezo alionao.
0 COMMENTS:
Post a Comment