Kocha wa makipa wa Simba,
James Kisaka, amemuweka chini kipa wake namba moja, Abel Dhaira ili wazungumzie
tatizo alilonalo na kutema mipira, lakini kipa huyo akaibua siri moja kubwa
inayosababisha tatizo hilo.
Kisaka amesema alilazimika
kuzungumza na kipa huyo, ambapo Dhaira ametaja sababu kubwa ni glovu
anazodakia.
“Ameniambia kuwa tatizo
kubwa ni glovu anazotumia ambazo hazina ubora unaotakiwa,” alisema Kisaka na
kuongeza:
“Dhaira amesema glovu
ambazo anatumia katika mazoezi wakati mwingine ndiyo hizo anazotumia katika
mechi, kitu ambacho siyo sahihi, lakini nimemweleza anatakiwa kuondoa hali hiyo
na hilo la glovu nitaliwasilisha kwa viongozi ili walishughulikie haraka.”
Matukio ya kutema mipira
mchezoni yamesababisha kuwe na hofu kubwa kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo kwa
kuwa hata katika mechi iliyopita dhidi ya Tanzania Prisons alifanya hivyo zaidi
ya mara moja.
0 COMMENTS:
Post a Comment