Klabu ya Simba imemtaka kiungo
mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa, aandae kabisa gari la kuzima moto kwenye
nyumba zake kwa kuwa ina uhakika mchezaji huyo hataweza kutimiza ahadi yake ya
kufunga au kutoa pasi ya bao.
Simba na Yanga zinakutana keshokutwa
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar na Ngassa ameahidi asipofunga au kutoa pasi
itakayozaa bao, basi atazichoma moto nyumba zake tano.
Ofisa
Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema hawana hofu na Ngassa na kwamba hana hata
historia ya kuifunga Simba, hivyo cha msingi aandae zima moto haraka ili
kuepuka hasara mapema.
“Siwezi kusema hatatufunga kwa kuwa ni
majaaliwa ya kila mtu jinsi Mungu alivyompangia lakini sisi hatuna hofu naye,
atambue kuwa hajawahi au hana historia ya kuifunga Simba, ila tunamshauri
aandae zima moto mapema, tusijemtia hasara bure,” alisema Kamwaga.
0 COMMENTS:
Post a Comment