November 2, 2013

AMROUCHE
 Kocha wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, Adel Amrouche amesema Didier Kavumbagu wa Yanga ana nafasi ya kuendelea kufanya vizuri zaidi.


Amrouche raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Algeria amesema mshambuliaji huyo wa Rwanda ana uwezo mkubwa na kocha anatakiwa kuendelea kumuamini.

“Didier ni kati ya washambuliaji bora katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati,” alisema Amrouche ambaye aliwahi kumfundisha alipokuwa kocha wa timu ya taifa ya Burundi kwa zaidi ya miaka mitatu.

“Ana uwezo wa kuchezesha timu akiwa mbele, mzuri wa vichwa na wakati mwingine anakuwa mtulivu sana katika umaliziaji.

“Nina imani atafanya vizuri zaidi na hata kama asipofunga, anakuwa mtoaji mzuri wa pasi za ufungaji kwa wenzake,” alisema.

Kavumbagu ni kati ya washambuliaji tishio katika Ligi Kuu Bara ambayo inaendelea na tayari Yanga imeshika usukani baada ya kuichapa JKT Ruvu mabao 4-0, jana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic