November 2, 2013


Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amesema hatakuwa na tatizo kama Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Bara, Yahaya Mohammed atataka kumtembelea ofisini kwake.


Manji amesema kawaida waungwana husikiliza kwanza wanachoelezwa kabla ya kuzungumza.

“Nitamkaribisha kama kweli atataka kunitembelea na kuzungumza na mimi. Sina tatizo katika hilo.

“Mazungumzo ndiyo yatatoa majibu ya kila mmoja wetu anachokitaka au kukiamini ni bora kwake na maendeleo ya mpira wa Tanzania,” alisema.

Hivi karibuni mara baada ya Yahaya kuchukua nafasi ya uenyekiti, alisema atamtembelea Manji ofisini kwake ili wazungumze kuhusiana na tofauti zilizojitokeza kati ya Yanga na bodi hiyo.

Bodi hiyo imeingia mkataba na Azam TV kuonyesha mechi za ligi kuu live, lakini Yanga imekuwa ikitaka kulipwa zaidi na kutaka kutofautishwa na timu nyingine ndogo ambazo hazina mashabiki wengine kama ilivyo yenyewe.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic