Rais aliyepita wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Leodeger Tenga amekabidhi fedha na mali ya jumla ya Sh bilioni
1.3 kwa rais mpya.
Rais Mpya wa TFF, Jamal Malinzi
amekabidhiwa vitu hivyo leo katika ofisi za shirikisho hilo Karume, Ilala
jijini Dar es Salaam.
Katika vitu hivyo ni pamoja na eneo la
Krume lenye ukubwa wa ekari 8.2 ndani yake kukiwa na uwanja wa Karume, eneo la
ekari 19 lililo mkoani Tanga na mahgari sita.
Katika akauti, TFF ina jumla ya Sh
milioni 33.5 na Tenga amesema fedha hizo zimebaki kiasi hicho baada ya kufanya
malipo ya mkutano mkuu Sh million 135, malipo ya maandalizi ya kikosi cha
Tanzanite Sh milioni 33.5 na yote yamefanyika ndani ya wiki tatu.
Lakini kati ya Jumanne au Jumatano,
malipo ya Sh milioni 664 kutoka TBL zitaingia ndani ya akaunti ya TFF na Juni
mwakani, idadi kama hiyo ya fedha itaingia tena.
Katika makabidhiano, Malinzi alismhukuru
sana Tenga na kusema ameonyesha juhudi kubwa nay eye anaahidi kuendelea kumuita
rais hata kama muda wake umekwisha.
0 COMMENTS:
Post a Comment