Kiungo wa Rhino Rangers ya Tabora, Nurdin
Bakari, amerejea katika kikosi hicho na kukatwa mshahara baada ya kushindwa
kuripoti kambini Tabora kwa wakati.
Kiungo huyo ambaye aliwahi kuichezea Yanga kabla ya msimu huu kutua katika kikosi hicho
cha jeshi, alichelewa kuripoti kambini bila kueleza sababu za msingi, hali
iliyosababisha uongozi umjadili.
Katibu
wa timu hiyo, Paul Maganga, alisema kiungo huyo amerejea na kuchukuliwa hatua
za kinidhamu ili asiweze kurudia tena.
“Uongozi umempatia barua ya kumuonya na
kumkata mshahara kwa siku ambazo amechelewa
kufika kambini na kuungana na wenzake. Kwa sasa tayari amesharejea.
“Lakini baada ya kumpatia barua, tunashukuru
naye aliweza kuandika barua kwetu kwa ajili ya kuomba msamaha na kueleza yale
ambayo yalimkwamisha kufika kwa wakati,” alisema Paul.
0 COMMENTS:
Post a Comment