Uongozi wa Uwanja wa Sokoine wa mkoani
Mbeya, umesema umetumia zaidi ya shilingi milioni 22.3 kwa ajili ya ukarabati
wa uwanja wao.
Uwanja wa Sokoine unaotumiwa na timu za
Mbeya City na Tanzania Prisons, ulifungiwa na TFF kutokana na kutokidhi viwango
vya kuchezea ligi kuu.
Meneja
wa uwanja huo, Modestus Mwaruka, alisema uwanja huo ulichukua mwezi mmoja hadi
kuwa sawa na wametumia kiasi cha milioni 22 kwenye sehemu ya kuchezea ‘pichi’
tu.
Alisema gharama hizo ni za ununuzi wa
nyasi za asili vipande 99 pamoja na usafiri na wanaamini utadumu sana kwa kuwa
upandwaji wake ulizingatia kanuni za upandwaji ambapo zitakapoota, uwanja huo
unaweza kuchezewa hata mechi za kimataifa.
“Tumemaliza kazi tuliyopewa ya
kurekebisha uwanja wetu na tumetumia milioni 22 na zaidi, tumeboresha sehemu ya
waamuzi, vyoo na majukwaa, sasa hivi hata mechi za kimataifa zinaweza kuchezwa
hapa,” alisema Mwaruka.
0 COMMENTS:
Post a Comment