Klabu ya Lipuli ya Iringa, imesema
imefuta mpango wa kumfungulia mashtaka aliyekuwa kocha wao Shadrack Nsajigwa, baada
ya kocha huyo kutimkia Nepal.
Nsajigwa anatuhumiwa kukimbia klabu
hiyo, akiwa amekaa klabuni hapo kwa miezi miwili wakati akiwa na mkataba wa mwaka
mmoja, hivyo Lipuli walitaka walipwe fidia.
Katibu wa Lipuli, Willy Chikweo, alisema mpango wa kumuweka ndani beki huyo wa
zamani wa Yanga, wameachana nao kwa kuwa amekimbilia nje ya nchi.
“Tumekubaliana kumsamehe, maana kwanza
tunasikia alikimbilia Nepal. Pili, familia yake inaishi kwa kutegemea ajira hii
ya soka, hivyo tuliona tukimshtaki tutakuwa tunahatarisha maisha ya familia
yake, kwa sababu alitakiwa atulipe sisi miezi iliyobaki na tunajua hana hiyo
hela,” alisema Chikweo na kuongeza kuwa, msamaha huo pia unamhusu kiungo
Godfrey Bonny aliyetoweka klabuni.
0 COMMENTS:
Post a Comment