September 9, 2014

Mashabiki Simba wameonyesha furaha yao kubwa kuhusiana na mshambuliaji Emmanuel Okwi kushinda kesi yake na kuruhusiwa kuichezea Simba.

Mashabiki hao walimgombea Okwi katika mazoezi ya Simba, Bunju Ununio jijini Dar.
Mara tu baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo, mashabiki hao walimgombea Okwi kila mmoja akitaka kumgusa au kupiga naye picha.

Waliimba nyimbo za kumkaribisha nyumbani huku wakiikebehi Yanga.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, imemrejesha Okwi kuichezea Simba licha ya Yanga kudai amekiuka mkataba.
Hata hivyo, tayari Yanga iko kwenye utaratibu wa kukata rufaa kupinga uamuzi huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic