Baada ya
kufanikiwa kubeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na Copa del Rey, Real
Madrid imetangazwa kuwa klabu bora ya Ulaya.
Madrid
imetangazwa kuchukua tuzo hiyo kubwa zaidi kwa klabu barani Ulaya na Chama cha
Klabu za Kulipwa Ulaya (Eca) katika hafla ya tuzo iliyofanyika mjini Geneva,
Uswiss, leo.
Tuzo hiyo
ilipokelewa na Makamu wa Rais wa Real Madrid, Pedro López na mkurugenzi wa
taasisi ya uhusiano bora ya klabu hiyo, Emilio Butragueno.
Red Bull
Salzburg ilishinda tuzo ya klabu inayochipukia kwa mafanikio ya juu na Celtic
ya Scotland ikabeba tuzo ya iliyofanikiwa zaidi kimasoko.
0 COMMENTS:
Post a Comment