Kama mshambuliaji wa Yanga, Geilson Santos
Santana ‘Jaja’ na kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Andrey Coutinho ambao ni raia
wa Brazil wangetumia vyema nafasi walizozipata kufunga mabao, basi uongozi wa
timu hiyo ungetoa shilingi milioni 80 kwao.
Wabrazili hao walikosa nafasi hizo za wazi
wakati timu yao ilipovaana na wapinzani wao, Simba, katika mechi ya Ligi Kuu
Bara ambayo ilimalizika kwa suluhu.
Jaja na Coutinho walikosa mabao hayo wakiwa
wamebaki wao na kipa ndani ya sita wakishindwa kumfunga kipa chipukizi, Peter Manyika
Jr.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani
ya benchi la ufundi la timu hiyo, wachezaji hao kabla ya mechi hiyo waliahidiwa
kupewa fedha hizo kama morali endapo watawafunga watani wao wa jadi Simba.
Chanzo hicho kilisema, fedha hizo waliahidiwa
siku moja kabla ya mechi wakati viongozi walipoitembelea kambi ya timu hiyo
iliyoweka Landmark, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
“Wachezaji
wameikosa ahadi waliyopewa na viongozi wao, kabla ya mechi na Simba viongozi
walikwenda kambini Mbezi Beach kwa ajili ya kwenda kuwatembea pamoja na kula
chakula cha usiku.
“Waliahidiwa kupewa mil. 80 zilizopangwa
kugawanywa kwa kuanzia kwa wachezaji na benchi zima la ufundi,” kilisema chanzo
hicho.
0 COMMENTS:
Post a Comment