Kipa wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’
amesema kipa kinda wa Simba, Peter Manyika, ndiye anastahili kuwa mchezaji bora
wa mechi yao ya Jumamosi.
Dida alifunguka kuwa kama angepewa nafasi ya
kuchagua mchezaji bora wa mechi katika mchezo wa juzi kati ya Yanga na Simba,
bila kipingamizi angempa tuzo yosso huyo wa miaka 18, kauli iliyoungwa mkono na
kipa mkongwe nchini, Juma Kaseja.
DIDA |
Manyika ambaye ni mtoto wa kipa wa zamani wa
Yanga na Taifa Stars, Manyika Peter, alikuwa gumzo uwanjani hapo kwa kiwango
kizuri alichoonyesha huku akichomoa michomo mikali, ukiwemo wa Andrey Coutinho
ambaye walikuwa uso kwa uso langoni.
KASEJA |
“Lazima tuseme ukweli Manyika amefanya kazi
kubwa ambayo hakuna aliyeitarajia katika mchezo mkubwa kama huu, hata mimi
sikutarajia kama angeweza kufanya vile na ninaweza kusema kuwa alikuwa ‘man of
the match’ kwa ukweli ulio wazi,” alisema.
Wakati huohuo, Kocha wa Simba, Patrick Phiri,
amekiri kwamba Manyika ndiye aliyekuwa mchezaji bora kwenye mechi hiyo ya
watani juzi.
“Kwa upande wangu Manyika ndiye mchezaji bora
katika mechi ya leo (juzi), ukiangalia ameokoa mipira mingi yeye akiwa na
washambuliaji wa Yanga ndani ya 18.
“Isitoshe mechi hii ni ya kwanza kwake kwenye ligi
kuu tukiwa tunakutana na Yanga, ninampongeza sana Manyika amecheza vizuri sana,”
alisema Phiri.
0 COMMENTS:
Post a Comment