Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo ameondoka nchini leo alfajiri kurejea kwao Brazil.
Maximo ameondoka pamoja na kocha msaidizi, Leonaldo Leiva ambaye pia ni raia wa Brazil.
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu amesema wakati kocha huyo akiwa Brazil, wachezaji wa Yanga wamepewa siku kumi za mapumziko.
"Wachezaji watapumzika kwa siku kumi, baada ya hapo wataitwa tena kuungana kwa ajili ya kuanza kazi," alisema Njovu.
Ligi Kuu Bara imesimama hadi Desemba 27 na Yanga ilimaliza mchezo wake wa saba kwa kuitwanga Mgambo kwa mabao 2-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment