Mshambuliaji wa Polisi Moro, Daniel
Mwarwanda maarufu kama Danny Mrwanda amefunga mabao mawili na kusaidia timu
yake kuichakaza JKT Ruvu kwa mabao 2-1.
JKT Ruvu inayonolewa na Fred Felix Malinzi,
mechi yake iliyopita ilikuwa imepata ushindi dhidi ya Azam FC.
Hivyo ikaingia uwanjani ikitaka kuongeza
ushindi wa pili kwenye Uwanja wa Azam Complex lakini nguvu yao haikutosha
kuizuia Polisi.
Bao pekee la JKT Ruvu lilifungwa na Jafar
Kisoki ambao walitangulia kufunga, kabla ya Mrwanda kuwaadhibu mara mbili.
0 COMMENTS:
Post a Comment