Mwamuzi kutoka Tanzania, Samwel
Mpenzu, amefuzu kuchezesha michuano mikubwa itakayoandaliwa na Shirikisho la
Soka Afrika (Caf) ikiiwemo ya Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa
miaka 20 (Afcon U-20).
Mpenzu, ambaye ni mwamuzi mwenye beji
ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), amefuzu baada ya kupita kwenye
mchujo wa kupata nafasi hiyo ambao ulifanyika Cairo, Misri wiki iliyopita
pamoja na waamuzi wengine kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.
Mwamuzi huyo alisema kuwa baada ya kupita kwenye
hatua hiyo, kwa sasa anachoangalia ni kupita kwenye hatua inayofuata ‘Elite A’
ambayo itamfanya aweze kuchezesha michuano ya wakubwa ya Afcon pamoja na Kombe
la Dunia.
Alisema kuwa lengo lake kubwa ni
kuchezesha Kombe la Dunia, kwani hakuna Mtanzania aliyefika huko.
0 COMMENTS:
Post a Comment