Shabiki mmoja wa Klabu ya Yanga ambaye
jina lake halikupatikana haraka, ‘alikunwa’ na uwezo wa mlinda mlango wa timu
hiyo, Deogratius Munishi ‘Dida’ na kujikuta akipagawa na kuamua kumkodishia
bodaboda staa huyo.
Hayo yalijiri mara baada ya programu
ya mazoezi ya Yanga yaliyofanyika wikiendi iliyopita kwenye Viwanja vya Shule
ya Sekondari Loyola, Dar ambapo wachezaji wa timu hiyo walikuwa ‘wakichomoka’
kwenda kwao.
Programu hiyo ilipomalizika, wachezaji
walikuwa wakitoka uwanjani hapo kila mmoja akiwa na usafiri wake, lakini Dida
alipotoka kwenda kutafuta usafiri, shabiki huyo alijitokeza na kumlipia
bodaboda.
“Wewe bodaboda chukua pesa hii,
mpeleke huyu jamaa tena kwa mwendo wa kifalme, tuna mechi na Simba inakaribia.
“Umfikishe hadi Jangwani, sasa ole
wako ukamshushie Msimbazi,” alibwata shabiki huyo huku akimkabidhi dereva wa
bodaboda noti ya shilingi elfu mbili.
Mara baada ya makabidhiano hayo, Dida
alidandia bodaboda na safari ikaanza kwa mwendo wa taratibu.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment