RUVU |
Klabu ya Ruvu Shooting ya Pwani, imeamua kumwaga nyota watano kwa mpigo
katika harakati za kutafuta mastraika, safu ambayo imewasumbua kwa muda mrefu tangu
kuondoka kwa Elias Maguli aliyetimkia Simba.
Ofisa Habari wa Ruvu, Masau Bwire, alisema nyota hao tayari wameanza
majaribio tangu juzi Jumatatu ambapo wataangalia wenye uwezo zaidi kabla ya
kuwapa saini.
Bwire amesema kuwa wameamua kuvalia njuga safu hiyo kwani ndiyo
iliyoonyesha matatizo zaidi katika mechi saba za mzunguko wa kwanza.
“Kuna wachezaji watano wameanza mazoezi na kikosi chetu, wanatokea timu
ndogo, wapo kwa ajili ya majaribio ambapo kocha Tom Olaba atapata nafasi ya
kuchagua nani atavutiwa naye.
“Tumeamua kuleta mastraika maana ndiyo sehemu iliyotutesa zaidi na
ikumbukwe kuwa kuna wachezaji wetu kama saba ambao wamekwenda kwenye mafunzo ya
kijeshi, hivyo tunataka kuziba mapengo yao,” alisema Bwire ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Uchaguzi wa Chama cha Soka Mkoa wa Pwani (Corefa).
0 COMMENTS:
Post a Comment