February 22, 2015



MPIRA UMEKWISHAAAAAAAAAA.........
Dk 90+3 Mrwanda naye analambwa kadi ya njano kutokana na kucheza rafu kwa kukusudia

Dk 90+2 Cannavaro anafanya kazi ya ziada kuokoa krosi ya Mwasapili.
Dk 90, Mapunda analambwa kadi ya njano kwa kumchezea faulo mbaya Mrwanda.

Dk 88 Mapunda anapata pasi nzuri lakini shuti lake hafifu linadakwa kiulaiiiniii na Barthez

Dk 82 Mwagane Yeya anaingia kuchukua nafasi ya Felix

GOOOOOOOO Kona safi iliyochongwa na Niyonzima, inatua kichwani mwa Tambwe anafunga bonge la bao.....

Dk 77, Kenny Ally anaingia kuchukua nafasi ya Alfa
Dk 76 Said Juma Makapu anaingia kuchukua nafasi ya Telela...
Dk 70, Cannavaro analala kuokoa tena krosi nzuri ya Kaseke na City wanaonekana kutawala mchezo
Dk 69, Mwamuzi anampa Felix kadi ya njano....
GOOOOOOOOOOOO  Dk 68, Peter Mapunda anaruka na kufunga bao zuri kwa kichwa kuwahi krisi nzuri ya Felix.



Dk 67 Kipa Burhani anaokoa vizuri krosi ya Ngassa
Dk 67 Cannavaro analala na kuondosha mpira wakati Felix akiambaa
Dk 64 Msuva anapiga kichwa, mpira ukiwa anakwenda wavuni, beki anawahi na kuuondosha. Ilikuwa ni baada ya kipa na beki wake kuchanganyana

  GOOOOOOOOO Dk 59, Ngassa anampiga chenga kipa Burhani aliyejaribu kumpiga chenga yeye na kuandika bao la pili kwa Yanga kwa ufundi kabisa...
Dk 58 faulo nzuri ya Felix lakini wachezaji wengine wa City wanashindwa kumalizia
Dk 55, Danny Mrwanda anaingia kuchukua nafasi ya Coutinho.

Dk 52 Coutinho anaomba kutoka baada ya kuumia, alitibiwa na kurudi uwanjani. Lakini baadaye akalazimika kutoka nje baada ya kuomba
Dk 46, Yanga wanaanza kwa kufanya shambulizi, Ngassa anashindwa kuwa makini lakini City wanajibu. Mbunge wa Mbeya Mjini, Sugu yuko jukwaani anaendelea kuhamasisha mashabiki wa City


MAPUMZIKO
Dk 42 City wanagongeana vizuri lakini shuti la Nonga linakuwa halina macho.


Dk 38 Juma Abdul analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Themi Felix.
Dk 36, Mbeya City wanacheza vizuri na kinda Raphael Alpha anapiga shuti kali lakini linatoka nje kidogo

Dk 35, Simon Msuva anapiga krosi nzuri baada ya mabeki wa Mbeya City kufanya uzembe, lakini kipa anakuwa mwepesi kuwahi.
DK 26 HADI  31 zaidi mpira unachezwa katikati ya uwanja

Dk 24, mpira wa krosi wa Joshua unatua kichwani kwa Msuva, anapiga vizuri lakini unapita juu kidogo.
Dk 20 Mwamuzi Lazi anamuonya Telela kwa kucheza faulo mara kwa mara....lakini hakumpa kadi

GOOOOOOOOO DK 18 Msuva anaruka juu kuiwahi pasi nzuri ya Niyonzima na kufunga bao safi la kichwa....
Dk 12 Paul Nonga anapiga kichwa lakini kinadakwa kwa ulaiini na Barthez.

Dk 5 Themi Felix anautupia mpira wavuni lakini mwamuzi anasema alishika kabla ya kufunga
Dk 4, krosi safi ya Juma Abdul inatua mikononi mwa kipa wa Mbeya City.

Dk 1Yanga wanakuwa wa kwanza kufanya shambulizi, Niyonzima napiga shuti linatoka nje.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic