Mashabiki mbalimbali wa klabu ya Yanga wanaanza
safari leo kuifuata FC Platinum ya Zimbabwe.
Yanga itashuka dimbani katika ardhi ya Zimbabwe
kuivaa timu hiyo katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho baada ya kuwa
imeshinda 5-1 katika mechi ya kwanza jijini Dar.
Mashabiki hao kwa kutumia basi dogo aina ya Toyota Coaster watapitia Mbeya, Tunduma tayari
kwa ajili ya kwenda kuishangilia Yanga katika mechi itakayopigwa Jumamosi.
Yanga inatarajia kuondoka kesho kwa ndege ya kukodi
ya serikali, tayari kuwavaa FC Plutinum.
Pamoja na Yanga kuwa imeshinda kwa mabao 5-1,
bado mechi hiyo inaonekana itakuwa ni ya ushindani mkubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment