AME ALI. |
Kama bado kuna mchezaji
raia wa Tanzania anawaza kuichezea Azam FC kwa msimu ujao aandike imekula kwake
kwani timu hiyo imefunga usajili kwa wachezaji wa ndani pindi tu ilipomnasa Ame
Ally kutoka Mtibwa Sugar.
Kwa sasa Azam ina majina
ya nyota kadhaa wa kigeni inayotaka kuwasajili lakini wanasubiri tu kauli ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya idadi ya nyota wa kigeni kikosini.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Azam, Saad Kawemba amesema Zungu ndiye mchezaji wa
mwisho kujiunga nao na walimhitaji kwa muda mrefu.
“Labda litokee tatizo tu
lakini tumeshafunga usajili kwa wachezaji a ndani na sasa tunasubiri kauli ya
TFF kama itaongeza idadi ya wachezaji wa kigeni tuwasajili tulionao,” alisema
Kawemba.
Alisema katika orodha yao
kuna wachezaji kutoka Afrika Magharibi na Kusini ambao watasajiliwa pindi ruksa
itakapotoka ya kusajili wachezaji kumi wa kigeni.
Wakati huohuo, wachezaji
wawili kiungo Bamidele-tope Julius kutoka Nigeria na Laurent Raphael kutoka
Kayanga FC ya Kagera wanafanya majaribio katika kikosi hicho.
0 COMMENTS:
Post a Comment