Pamoja ya kuwepo kwenye mchakato wake wa uchaguzi mkuu ambao
unatarajia kufanyika mapema Julai 5, mwaka huu, Kamati ya Usajili ya Coastal
Union, inaendelea na mazungumzo na wachezaji kadhaa akiwemo mshambuliaji wa
Stand United, Mnaigeria, Abasirim Chidiebere.
Tayari kikosi hicho kimefanikiwa kunasa saini ya wachezaji
takriban watatu, ambao ni straika Ahmed Shiboli, kipa Benedict Haule na
mshambuliaji chipukizi Mohammed Mtiti huku ikiwafungia virago nyota wake kadhaa
ambao walikuwa wamemaliza mikataba yao.
Chidiebere amesema ni kweli tayari yuko katika mazungumzo na
Wagosi wa Kaya.
“Ni kweli nimefuatwa na Coastal kwa ajili ya mazungumzo,
tunaendelea ila bado hatujaafikiana lakini pia Mbeya City na hata Kagera Sugar
japo walipiga tu simu kuwa wananihitaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment