TINOCCO AKIWA MAZOEZINI YANGA. |
Kipa mpya wa Klabu ya Yanga, Benedict Tinoco amesema amechagua
kuvaa jezi namba 29 ambayo ilikuwa ikivaliwa na Juma Kaseja huku akiweka wazi
sababu za kuikataa ile ya kipa wa akiba, Deogratius Munishi ‘Dida’.
Tinoco ambaye aliwahi kuwa kipa bora kwenye Michuano ya Copa
Coca-Cola, amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Kagera Sugar
ambako alikuwa amemaliza mkataba.
Tinoco ambaye ni chimbuko la mpango wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) wa Maboresho alisema, awali alipenda kuvaa jezi namba 30, lakini kwa kuwa
inavaliwa na mwenzake Dida ambaye ana jina kubwa klabuni hapo, ameamua kubadili
mawazo na sasa anaitaka namba 29.
Tinoco ambaye msimu uliopita aliichezea Kagera mechi sita na
kufungwa mabao manne, alisema amechagua jezi ya Kaseja kwa kuwa anamkubali na
anahisi kama atakuwa anamuona kwenye ulimwengu wa soka.
“Jezi ninayoipenda ina mtu na mwenye hiyo jezi ni kipa ambaye
ninamheshimu sana katika nchi hii ambayo ni 30 na inavaliwa na Dida, ila hakuna
tatizo nitavaa ile ya Kaseja (29) kwani naye namkubali sana na ni mmoja wa makipa
bora katika soka la Tanzania, najua kila mmoja angetamani kufikia mafanikio
yake,” alisema Tinoco.
0 COMMENTS:
Post a Comment