August 15, 2015

SIMBA ILIYOANZA LEO, KERR AKABADILI WACHEZAJI SABA KATIKA KIPINDI CHA PILI.

Simba imeibuka na ushindi  wa mabao 2-1 dhidi ya URA ya Uganda ambayo imekuwa ikiwafunga kila inapocheza nao.


Simba imeibuka na ushindi wa mabao hayo ikiwa na wachezaji baada ya Peter Mwalyanzi kuumia huku Kocha Dylan Kerr akiwa amemaliza sub zote, hivyo Simba ikaendelea kupambana ikiwa na wachezaji 10 uwanjani.

Mara zaidi ya tatu, Simba imekuwa ikilala kutoka kwa URA kwa misimu minne sasa.

Hivyo ushindi wa leo, Simba ilikuwa imemaliza uteja kutoka kwa wakusanya mapato hao wa Uganda.


Mashujaa wa Simba leo ni Mganda Juuko Murshid na Mrundi, Kelvin Ndayisenga waliofunga mabao hayo mawili wakati Simba ikiamka katika kipindi cha pili baada ya kuonekana imelala katika kipindi cha kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic