August 15, 2015


Ili kujiandaa vizuri kuhakikisha inaishinda Nigeria mwezi ujao, Taifa Stars itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Oman.


Taifa stars itasafiri hadi Muscat, Oman kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Oman.

Gazeti la Oman la Oman Newspaper limeripoti kocha wa Oman akionyesha kufurahishwa na mechi mbili za kirafiki.
STARS

Kocha huyo amesema mechi yake ya kwanza itakuwa Agosti 24 dhidi ya Tanzania kabla ya kuivaa Yemen Agosti 28.

Juhudi za kuwapata watu wa TFF kuthibitisha zilikuwa ngumu, lakini taarifa nyingine za ndani zimethibitisha.

“Kweli nimesikia timu wakati inakwenda Uturuki itaanzia Oman kwanza kwa ajili ya mechi hiyo ya kirafiki.


“Baada ya hapo itaendelea na safari kwenda Uturuki ambako itaweka kambi. Lakini bado sijapata uhakika wa hilo,” kilieleza chanzo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic