Azam FC leo Jumamosi inaanza harakati za kusaka ubingwa wa Ligi
Kuu Bara lakini ina pigo la kuwakosa nyota wake wawili, Shomari Kapombe na
Michael Bolou.
Wachezaji hao watakuwa jukwaani katika uwanja wao wa Azam Complex
uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam wakiishuhudia timu yao ikicheza dhidi ya
Prisons ya Mbeya.
Kwa mujibu wa Daktari wa Azam, Twalib Misuli, Kapombe aliumia
kifundo cha mguu juzi Alhamisi wakiwa katika maandalizi ya mchezo huo na
Prisons wakati Bolou yeye tatizo lake la goti ni la muda mrefu.
“Kapombe bado hali yake haijawa katika hali ya ushindani, kwani
ameumia mguu wa kulia na hataweza kucheza, tunaogopa kulazimisha acheze kwa
kuwa anaweza kuumia zaidi.
“Huyu Bolou yupo katika programu maalum kuhusu goti lake na
ataendelea kuwa chini ya uangalizi kwa muda hadi atakapokuwa vizuri kabisa ila
atarejea uwanjani hivi karibuni tu,” alisema Misuli.
Kapombe aliisaidia Azam kwa kiasi kikubwa katika michuano ya Kombe
la Kagame na kuiwezesha kutwaa ubingwa bila kuruhusu hata bao moja katika wavu
wake.









0 COMMENTS:
Post a Comment