September 12, 2015


Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Said Bahanuzi, ameibuka na kusema wapinzani wao katika Ligi Kuu Bara wasitambe sana kwani watawaumbua kwa kuwafunga  kutokana na kuwa na kikosi bora.


Bahanuzi aliyetupiwa virago na Yanga, amesema atapigana kufa na kupona kuhakikisha anaisaidia timu yake kufanya vizuri katika michezo yote ya ligi.

Alisema timu pinzani kwao kama Simba, Yanga na Azam FC, zimekuwa na mazoea ya kusifu vikosi vyao wakati uwanjani hucheza soka la kawaida sana na amepania kuziadabisha.

“Mtibwa ipo vizuri kwa kuleta ushindani kwenye ligi na kwa upande wangu, nimejipanga kurejesha makali yangu niliyokuwa nayo kabla ya kwenda Yanga.

“Najua hizo timu kubwa zinatamba kila siku kuwa na vikosi imara, lakini najua tutakachozifanya na hilo litakuwa fundisho kwao kudharau wachezaji zilizokuwa nao,” alisema Bahanuzi.

Katika kikosi cha Mtibwa, Bahanuzi yupo na Hussein Javu ambaye walikuwa wote Yanga lakini hawakuweza kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic