September 12, 2015

MAJIMAJI

Majimaji imerudi Ligi Kuu Bara na imeanza kazi, imeitwanga JKT Ruvu kwa bao 1-0.


Ushindi wa kwanza kwa Majimaji ambayo imerejea Ligi Kuu, umepatikana baada ya timu hiyo kuitwanga JKT kwa bao hilo moja kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Wakati Majimaji wanaowaonyesha kazi wanajeshi hao, Mbeya City iliyomsajili Juma Kaseja msimu huu, imekubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wageni wake, Kagera Sugar.

Licha ya Mbeya City kushambulia mfululizo katika kipindi cha pili wakionyesha wamepania kusawazisha, lakini Kagera walionekana kuwa imara kwa kucheza soka la mpangilio na kujipanga vizuri katika safu ya ulinzi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic