| LIEWIG |
Timu zote za mkoa wa Shinyanga zimeanza kwa kipigo katika mechi zao za ufunguzi wa Ligi Kuu Bara.
Mwadui FC inayofundishwa na Jamhuri Kihwelo 'Julio' ikiwa ugenini CCM Kirumba jijini Mwanza imetandikwa bao 1-0 na wenyeji Toto African.
Mwadui FC ambao walisafiri kilomita 224, wangeweza kupata bao la kusawazisha baada ya kupata penalti, lakini Nizar Khalfan akapiga mnazi.
Kwa upande mwingine, Stand United wakiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga imejikuta ikilala kwa bao 1-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar.
Kocha wa zamani wa Simba, Patrick Liewig raia wa Ufaransa ndiye anayeinoa Stand United.







0 COMMENTS:
Post a Comment