Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
anatarajiwa kukutana wazazi wa vijana wenye umri chini ya miaka 13 (U-13)
waliochaguliwa kujiunga na kituo cha michezo cha Alliance kilichopo jijini
Mwanza.
Malinzi anatarajiwa kukutana na wazazi wa vijana hao siku ya
jumatatu ya tarehe 14, Septemba 2015 saa 5 kamili asubuhi katika shule ya
Alliance, kabla ya taratibu za kuwakabidhi vijana hao kwa uongozi wa kituo
hicho.
Mapema
mwezi Juni mwaka huu TFF iliendesha mashindano ya Taifa kwa vijana wenye umri
chini ya miaka 13 (U-13) yaliyofanyika jijini Mwanza, ambapo jopo la makocha
liliweza kuchagua wachezaji 20 wenye vipaji ambao watajiunga na kituo hicho kwa
ajili ya masomo ya kawaida na kufundishwa michezo.
Mpango
huo wa kuwaweka vijana katika kituo cha Alliance una lengo la kuandaa timu bora
ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17, itakayoshiriki kwenye Fainali
za Mataifa ya Afrika kwa Vijana wenye umri huo zitakazofanyika nchini Tanzania
mwaka 2019.
IMETOLEWA NA TFF.







0 COMMENTS:
Post a Comment