November 11, 2015


 Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema mechi dhidi ya vijana wa Afrika Kusini chini ya miaka 23 ilikuwa mazoezi bora kabisa kama kipimo.


Lakini akasema wachezaji wake walishindwa kuwa wepesi kutokana na mazoezi makali waliyokuwa wakifanya.

“Tumefanya mazoezi makali kwa zaidi ya siku nne. Tayaribu tumekwenda tunapunguza na ndiyo tunaendelea hivyo,” alisema Mkwasa.



“Timu ya taifa ya vijana ya Afrika Kusini ni nzuri sana, wachezaji wengi ni mastaa katika timu za Ligi Kuu Afrika Kusini, pia dakara la kwanza. Hivyo ni mazoezi bora kwetu.”

Katika mechi hiyo ambayo Stars ililala kwa mabak 2-0. Vijana hao walikitawala kipindi chote cha kwanza na kuwapa Stars wakati mgumu.

Angalau katika kipindi cha pili, Stars ilionekana kubadilika taratibu hadi ilipofanikiwa kupata bao kupitia kwa Elius Maguri, wakati mwamuzi wa kati akiamini ni bao, mwamuzi msaidizi akasema hapana.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic