Kocha Msaidizi wa timu ya vijana ya Afrika Kusini chini ya
miaka 23, Shaun Bartlett amesema kikosi cha Tanzania, Taifa Stars kina uwezo wa
kuitoa Algeria lakini haitakuwa lahisi.
Kikosi cha Barltett ambacho Kocha Mkuu ni Owen Da Gama kiliifunga Stars kwa mabao 2-0
katika mechi mazoezi ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa Eldorado jijini
Johanneburg, jana.
Bartlett amesema Algeria ni timu bora na yenye
wachezaji wazoefu, lakini katika soka mambo hubadilishwa na wanaojiamini na
kujituma.
“Utulivu linakuwa ni jambo namba moja, lazima kile
ambacho wachezaji wameagizwa na mwalimu na wanajua ni kipi cha kufanya basi
kifanyike kwa uhakika.
“Kwanza kabisa lazima wachezaji wajiamini kuwa wana
kazi kubwa kubwa na inawezekana. Wakiingia uwanjani wanaamini haiwezekani,
ndiyo itakuwa hivyo,” alisema Bartlett aliyewahi kuichezea Charton Athletics iiliyokuwa
inashiriki Ligi Kuu England.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Bafanabafana amesema
mabadili katika mchezo wa soka ni timu ndogo kuifunga timu kubwa.
“Kama timu kubwa zitaendelea kufanya vizuri dhidi ya
timu ndogo, maana yake hakuna mabadiliko. Matokeo yasiyotarajiwa ndiyo
mabadiliko. Yakitokea ndiyo yanaongeza radha ya soka na lazima yafanywe na
wanaojiamini kuwa inawezekana.”
Stars inaivaa Algeria Jumamosi jijini Dar es Salaam,
katika mechi inayotarajiwa kuwa kali na ya kusisimua.
0 COMMENTS:
Post a Comment