November 11, 2015


Washambuliaji wawili wa TP Mazembe, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanatarajia kutua jijini Dar es Salaam, leo.


Samatta na Ulimwengu wataungana na Stars leo jioni kwa kuwa kikosi hicho kinatarajia kutua jijini Dar es Salaam leo saa 12 jioni kikitokea Afrika Kusini kilipoweka kambi ya zaidi ya wiki moja.

Samatta na Ulimwengu walikuwa DR Congo ambako waliiongoza TP Mazembe kubeba ubingwa wa Afrika na kuwa Watanzania wa kwanza kuvaa medali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Stars utawasili hiyo jioni kwa ndege ya Fast Jet na moja kwa moja itakwenda kambini kufanya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mechi dhidi ya Algeria itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic