Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Bara
‘Kilimanjaro Stars’, Abdallah Kibadeni, amesema ana uhakika kikosi chake
kitafanya vizuri kwenye Kombe la Chalenji bila ya nyota Mbwana Samatta na
Thomas Ulimwengu.
Kilimanjaro Stars itacheza mechi yake ya kwanza
kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Addis Ababa dhidi ya Somalia jijini Addis
Ababa, Ethiopia.
Samatta, Ulimwengu wa TP Mazembe ya DR Congo na
kiungo Mrisho Ngassa wa Free State Stars ya Afrika Kusini, hawapo katika kikosi
cha Kilimanjaro Stars na wamerejea katika klabu zao baada ya mchezo wa pili wa
Taifa Stars na Algeria kufuzu Kombe la Dunia 2018.
Nyota wengi wa Taifa Stars, ndiyo wanaounda
Kilimanjaro Stars na timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes.
“Ni pengo
kuwakosa Samatta, Ulimwengu na Ngassa, lakini nitajitahidi kuwatumia waliopo
kuhakikisha tunapambana kupata ubingwa.”
Katika moja ya mechi za leo kwenye Uwanja wa
Addis Ababa, Zanzibar Heroes iliyopo Kundi B itacheza na Burundi. Kesho katika
Kundi B, Kenya itacheza na Uganda.
Kilimanjaro Stars ipo Kundi A sambamba na wenyeji
Ethiopia, Somalia na Rwanda.
0 COMMENTS:
Post a Comment