Kocha Mkuu wa Simba, Dylan kerr amesema
ataendelea kutoa mazoezi makali kwa kikosi chake ili kurejesha ubora wa nguvu,
kasi na utimamu wa mwili.
Kerr amesema utimamu wa mwili utakuwa bora
zaidi kama mchezaji anakuwa fiti.
“Lazima wavumilie katika kipindi hiki, lazima
mazoezi yatakuwa makali sana kwa kuwa tunataka timu irejee vizuri.
“Baada ya hapo tutaendelea kupambana vilivyo
kuhakikisha tunaingia kwenye mambo mengine kama vile kufundishana mifumo na
nini cha kufanya.
“Tuna mechi nyingi ngumu mbele yetu, lazima
tufanye vizuri hivyo tunazidi kujiandaa,” alisema Kerr.
Simba imekuwa ikifanya mazoezi kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi maeneo ya Kunduchi jijini Dar es Salaam, mazoezi ambayo yameonyesha kuwapa wakati mgumu kutokana na ugumu wake.
0 COMMENTS:
Post a Comment