November 21, 2015


Akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya kwanza, Rais Dk. John Pombe Magufuli, jana amesema moja kati ya sekta atakazofanya nazo kazi kwa umakini ni michezo.


Magufuli alisema ameitaja sekta ya michezo kuwa ni miongoni mwa zinazopaswa kutazamwa kwa kina kwani ni moja kati vitu vinavyochangia maendeleo ya nchi.

Alisema atahakikisha sekta ya michezo inaboreshwa vilivyo ili iweze kuwanufaisha wananchi kwa kuwaongezea kipato kama ilivyo katika mataifa mengine duniani yaliyopiga hatua katika sekta hiyo.

“Yapo mambo mengi ya kuyaangalia na kuyafanyia kazi katika kipindi cha utawala wangu, moja kati hayo ni pamoja na sekta ya michezo na utamaduni.

“Tutahakikisha tunayafanyia kazi ili kuongeza wigo wa ajira kwa maendeleo ya taifa letu,” alisema Magufuli katika hotuba yake ya kuzindua rasmi bunge.


Kabla ya kuzindua bunge hilo, Magufuli alimuapisha Waziri Mkuu, Majaliwa Kasim Majaliwa asubuhi kwenye Ikulu ndogo ya Chamwino, Dodoma. Majaliwa ni mwanamichezo na ana taaluma ya ualimu wa soka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic