May 19, 2016

KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA VIJANA, SERENGETI BOYS KIMETINGA NUSU FAINALI YA MICHUANO YA VIJANA INAYOENDELEA NCHINI INDIA.

SERENGETI BOYS KIMEFANIKIWA KUPATA SARE YA MABAO 2-2 DHIDI YA KOREA KUSINI AMBAYO INAPEWA NAFASI KUBWA YA KUTWAA UBINGWA WA MICHUANO YA VIJANA INAYOENDELEA KWENYE MJI WA GOA NCHINI INDIA. NA NDIYO ILIYOWAPA NAFASI HIYO YA KUFIKA NUSU FAINALI.

MECHI ILIKUWA KALI NA BOYS WALIKUWA WA KWANZA KUPATA BAO KATIKA DAKIKA YA 12 MFUNGAJI AKIWA ASAD JUMA LAKINI KOREA KUSINI WAKASAWAZISHA KUPITIA SHIN SANGWHI.

KIPINDI CHA PILI MWANZONI KILIONEKANA CHA KOREA KUSINI NA WAKAFANIKIWA KUPATA BAO LA PILI KATIKA DAKIKA YA 58 MFUNGAJI AKIWA JOUNG SUNGJUNE.

HUKU MUDA UKIYOYOMA, IKIONEKANA KAMA KOREA WAMESHINDA, MAULID LEMBE AKAFUNGA BAO KATIKA DAKIKA YA 87 NA KUFANYA MATOKEO YAWE 2-2.
HII ILIKUWA NI MECHI YA TATU YA BOYS, WALIANZA KWA SARE YA BAO 1-1 DHIDI YA MAREKANI, WAKAWATWANGA WENYEJI INDIA BAO 3-1 KATIKA MECHI YA PILI.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV