July 12, 2016


Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema Medeama ya Ghana si timu ya kudharau na wanalazimika kujipanga kwenye mambo mengi sana.

Yanga inaivaa Medeama katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi.

Pluijm raia wa Uholanzi ambaye makazi yake yako nchini Ghana, amesema wapinzani wao pia ni timu bora.

“Timu inayofika katika hatua hii, haiwezi kuwa timu ya kubahatisha. Hatuwezi kuwadharau ndiyo maana tumekuwa na maandalizi ya juhudi kubwa.

“Tumeangalia makosa, tumeangalia vitu vya kuongeza na tunavifanyia kazi. Hakuna mjadala, tunataka kushinda na tunajua haiwezi kuwa rahisi,” alisema Pluijm.

Yanga iko kundi A na inashika mkia huku TP Mazembe ikiwa inaongoza na kufuatiwa na Mo Bejaia na Medeama.


.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV