July 12, 2016


SHUGHULI ZA KUSAINI MKATABA WA KWANZA
Uongozi wa Azam Media, leo unatarajia kumalizana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) pamoja na bodi ya ligi kuhusiana na mkataba mpya wa udhamini wa Ligi Kuu Bara.

Taarifa zimeeleza kuwa, baada ya mkataba wa awali kwisha, pande hizo zinatarajia kusaini mkataba mpya wa urushwaji live wa matangazo ya ligi kuu.


Azam Media ndiyo ilishinda na itaendelea kurusha Ligi Kuu Bara ingawa awali ilielezwa kulikuwa na figisu ambazo hata hivyo ziligonga mwamba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV